Stooyangu © 2025
Nyumbani > Masharti na Makubaliano ya matumizi >
1. Mtumiaji wa Stooyangu.com ® lazima awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, hii ni kwa ajili ya kuepuka usumbufu unaoweza jitokeza, tafadhali zingatia.
2. Mtumiaji wa Stooyangu.com ® ni lazima awe na akili timamu, hii ni kuepuka usumbufu na matatizo yanayoweza jitokeza.
3. Mtumiaji wa Stooyangu.com ® ni lazima awe anajua kuandika na kusoma, hii ni muhimu ili kuweza rahisisha mawasiliano.
4. Mtu yeyote anao uwezo wa kutumia Stooyangu.com ®, endapo amekidhi vigezo nambari 1, 2 na 3 vilivyo orodheshwa hapo juu.
1. Mpendwa mteja hakikisha taarifa zako unazo ziweka humu ni sahihi na za kweli, hii itasaidi kukuza uaminifu kati ya wauzaji na wanunuzi ndani ya Stooyangu.com ®, ili kufikia lengo letu la kukuza soko la ndani na kuboresha shughuli na huduma za kibiashara kupitia Stooyangu.com ®.
2. Mpendwa mteja hairuhusiwi kutumia huduma za Stooyangu.com ® kwa akaunti isiyo ya kwako (akaunti ya mtu mwingine), hii itapelekea kufungwa kabisa kwa akaunti hiyo husika.
3. Mpendwa mteja wewe ni mtu muhimu sana kwetu, hivyo tunawajibika kutunza taarifa zako binafsi na nyinginezo kama vile manunuzi na taarifa za shughuli mbalimbali unazo zifanya ndani ya Stooyangu.com ®. Hivyo ili kuendelea kuzilinda taarifa hizi hakikisha unatunza taarifa zako na usimpe mtu mwingine.
4. Mpendwa mteja ili kukuza ushirikiano na uaminifu katika shughuli mbalimbali ndani ya Stooyangu.com ®, hakikisha bishara utakayo ifanya ni halali (sio haramu) na iwe imethibitishwa na mamlaka husika.
5. Mpendwa mteja haturuhusu kuuza na kununua bidhaa hatarishi kama vile silaha, vifaa vilivyo chini ya kiwango, vyakula na madawa yaliyo kwisha muda wake, hii ni kwa ajili ya usalama wa watumiaji na afya zao, tunaomba usisite kutoa taarifa kwa yeyote atakaye patikana akikiuka sheria hii.
6. Mpendwa mteja, ukiwa kama mteja tunaomba usisite kutoa taarifa kama muuzaji uliye nunua bidhaa toka kwake hakukutendea haki, tafadhali toa taarifa mapema ili tuweze chukua hatua mapema ili kuendelea kudumisha uaminifu ndani ya Stooyangu.com ®.
7. Mpendwa mteja, ukiwa kama muuzaji ndani ya Stooyangu.com ®, unawajibu wa kumtumia mteja bidhaa yake pindi tu utakapo pokea malipo ya bidhaa hiyo. Kuchelewesha kutuma bidhaa bila sababu muhimu kutakupunguzia heshima na kupelekea kufungiwa stoo yako.
8. Mpendwa mteja haturuhusu matumizi ya lugha za matusi ndani ya Stooyangu.com ® au kuweka picha zenye maudhui yasiyo na maadili. Mfano kutangaza mavazi ya ndani, mavazi ya kimitindo n.k kunatakiwa kufanyike kwa kuzingatia maadili.
9. Mpendwa mteja haturuhusu matumizi ya taarifa za mtu mwingine bila ruhusa toka kwake, kama vile picha, kazi zenye hati miliki, Michoro, Nembo n.k.
Vigezo na masharti ya matumizi ya Stooyangu.com ® yanaweza badilishwa muda wowote ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu na pia kuendana na usalama, viwango na sheria mpya za matumizi ya kimitandao na mawasiliano pale itakapo tubidi. Ikitokea mabadiliko yamefanyika, wewe kama mteja wetu utatumiwa taarifa kukujulisha juu ya mabadiliko hayo mapya.
Ukiwa kama mteja wetu tunakuhakikishia kuwa taarifa unazoziweka katika Stooyangu.com ®, hazipelekwi wala kutumika sehemu nyingine yeyote nje ya Stooyangu.com ®. Taarifa hizi ni siri kati yako na sisi na hakutakuwa na mtu mwingine wa tatu. Tunajitahidi kuimalisha ulinzi katika mifumo yetu na hakikisha haumpi mtu yeyote tarifa zako.
Asante tunakutakia matumizi mema ya Stooyangu.com ®.