Stooyangu © 2025
Nyumbani > Kuhusu Sisi >
Stooyangu.com ni mtandao unao kupa urahisi wa kuuza na kununua bidhaa zako za kila siku mtandaoni kwa kutumia kompyuta na simu janja. Tunakurahisishia kufanya shughuli hizo kwa kukuunganisha na maelfu ya bidhaa za aina mbalimbali kutoka kwa stoo na wauzaji mbali mbali wa jumla na reja reja waliopo mikoa yote Tanzania.
Unaweza kutafuta bidhaa uzipendazo, kuangalia bei zabidhaa, kuangalia sifa za bidhaa, Kuangalia ofa za bidhaa toka kwa wauzaji mbalimbali, kuhifadhi machagulio ya bidhaa katika kapu la manunuzi, kuwasiliana na wauzaji, kupendekeza aina na sifa ya bidhaa unayo itaka, kufanya malipo ya bidhaa, kuangalia usafirishaji wa bidhaa n.k
Ukiwa kama muuzaji (mfanya biashara) Stooyangu.com inakurahisishia uuzaji wa bidhaa zako na kuwafikia wateja kiurahisi zaidi popote walipo nchini Tanzania bila kujali wapo karibu au mbali na sehemu yako ya biashara, na hivyo kupanua wigo wa biashara yako.
Stooyangu.com ni njia rahisi ya kuitangaza biashara yako, kutambulisha bidhaa mpya sokoni, kutangaza bidhaa unazo zalisha, ili ziwafikie wateja wengi zaidi waliopo sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Stooyangu.com inamilikiwa na kampuni ya ki Tanzania inayojishughulisha na teknolojia ya kimtandao na mifumo ya kompyuta, Yolim Enterprises Limited iliyo na makao yake makuu Dodoma, Tanzania.
Nyumbani > Kuhusu Sisi >