Ni taarifa gani binafsi zinazo muhusu mteja ambazo Stooyangu.com ® inazikusanya?
Tunakusanya taarifa zako binafsi kwa ajili ya kuzitumia katika kuboresha bidhaa na duduma zetu.
Mifano ya Taarifa binafsi tunazo kusanya:
Ni kwa malengo gani Stooyangu.com ® inatumia taarifa zako?
Tunatumia taarifa zako binafsi katika uendeshaji, utoaji, uendelezaji, na uboreshaji wa bidhaa na huduma ambazo tunazitoa kwa wateja wetu, malengo hayo yana husisha:
Manunuzi na usafirishaji wa bidhaa au huduma:
Tunatumia taarifa zako binafsi kuweza kushughulikia Oda zako, usafirishaji wa bidhaa na huduma, kurahisha shughuli za malipo na kuwasiliana na wewe juu ya Oda zako, bidhaa, huduma na ofa mbalimbali zinazo tolewa.
Kutatua changamoto na Kuboresha huduma:
Tunatumia taarifa zako binafsi ili kutoa suluhisho la matatizo mbalimbali yanayo weza jitokeza pindi utumiapo bidhaa na huduma zetu, ili kuhakikisha shida hizo haziendelei kutokea tena na kufanya huduma zote zitolewazo na Stooyangu.com ® kuwa rafiki zaidi ka watumiaji wetu.
Kutoa mapendekezo na utofauti wa huduma zetu:
Tunatumia taarifa zako binafsi ili kukupa mapendekezo ya huduma na bidhaa utakazo zipenda au unazo zipenda na kufanya utumie muda mchache zaidi kupata kile unachokitafuta na ukipendacho.
Kuweza kutimiza na kuendana na sheria za nchi:
Tunakusanyaa taarifa zako binafsi ili kutimiza mahitaji ya sheria za nchi hususani sheria za kimitandao ili kuzuia uhalifu au ubadhirifu wowote unaoweza jitokeza, kwa mfano tunakusanya taarifa za mteja ili kuweza mtambua na kumuhakiki kama ni mtumiaji halali an aliye timiza vigezo vya matumizi ya mtandao wetu.
Kuwasiliana na wewe:
Tunatumia taarifa zako binafsi ili kuwasiliana na wewe kuhusu huduma na bidhaa tunazozitoa, tunaweza fanya mawasiliano hayo kwa njia ya Simu au email.
Kwa jili ya Matangazo
Tunatumia taarifa zako binafsi ili kukuonyesha matangazo ya huduma na bidhaa ambazo zinaweza kuwa na mvuto kwako au zinazo weza kuhusiana na shughuli zako unazo zifanya kila siku.
Kwa jili ya Kuzuia udanganyifu na wizi
Tunatumia taarifa zako binafsi ili kuzuia wizi na udanganyifu unao weza kutokea pindi unapotumia huduma zetu kwa namna ambayo sio salama, tunafanya hivi ili kuwahakikishia wateja wetu ulinzi na usalama wa taarifa zao za kibenki na shuguli zao mtandaoni wanapo tumia huduma zitolewazo na Stooyangu.com ®.
Je vipi kuhusu Cookies na vitunza utambulisho vingine?
Ili kuwezesha mifumo yetu iweze kutambua ni aina gani ya brosa au kifaa unachotumia kuzifikia huduma zetu na kuimarisha huduma za Stooyangu.com ®, tunatumia cookies na vitambulisho vingine.
Je ni namna gani Stooyangu.com ® inasambaza taarifa zako?
Utunzaji wa taarifa kuhusu wateja wetu ni sehemu moja wapo muhimu sana ya biashara yetu, na hatuko kwenye biashara ya kuuza taarifa zako binafsi kwa watu wengine au kwa biashara nyingine, tuna sambaza taarifa zako kwa shughuli maalumu au utaratibu maalumu kwa ajili ya kutuwezesha kutoa huduma iliyo bora kwa watumiaji wetu huku tukizingatia faragha yako na ya taarifa zako kama ilivyo elezwa hapo chini.
Miamala inayo husisha makampuni mengine:
Unapofanya manunuzi au kulipia huduma na bidhaa utumiapo Stooyangu.com ®, taarifa zako binafsi ambazo ni muhimu kwa ajili ya muamala huo wa kifedha kufanyika zitatolewa kwa kampuni au biashara husika inayo shugulikia muamala huo ili uweze kuzitumia kukamilisha muamala huo.
Pindi tunapohitaji utekelezaji wa kazi fulani na kampuni au biashara nyingine:
Tunafanya kazi kwa kushirikiana na kampuni au biashara nyigine, pindi itakapo tubidi kufanya hivyo tunaweza toa baadhi ya taarifa zako kwa kampuni hiyo ili iweze kufanikisha kazi hiyo, kwa mfano tunapo safirisha mizigo kwakutumia kampuni nyingine itatubidi tuwapatie taarifa zako kama vile anwani, mawasiliano n.k. Tunaweza fanya hivyo pindi tu inapo hitajika na kwa kuzingatia sera ya faragha.
Pale inapotubidi kusambaza taarifa kwa vyombo, vitengo, mashirika au mamlaka za usalama za nchi:
Tunaweza sambaza baadhi ya taarifa za watumiaji wetu kwa vyombo, vitengo, mashirika au mamlaka za usalama za nchi pale inapotubidi na tutafanya hivyo kwa kuzingatia sheria na utaratibu wa nchi. Kama vile kitengo cha usalama, polisi, mahakama n.k
Zaidi ya hapo hututoweza sambaza taarifa kwa kampuni nyingine, na kama ikitokea basi utapokea taarifa ya ombi la kuturuhusu kufanya hivyo na unaweza kukubali au kukataa ombi hilo.
Ni namna gani taarifa zangu binafsi zipo salama?
Tumeitengeneza mifumo yetu kwa umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha tunaweka taarifa na shughuli zako salama.
Tunafanya kazi ili kulinda usalama wa taarifa zako binafsi kama vile kutuma taarifa zako kwa kutumia namna za vificho na mifumo mbalimbli ili zisiweze pokelewa na mtu asiye husika nazo.
Tunafuata taratibu zote katika kukamilisha miamala ya kifedha iwe ni kwa njia ya simu au kadi za benki, utaratibu kama Payment Card Industry Data Security Standards (PCI DSS).
Tunasimamia shughuli zozote zizonazo husiana na utoaji na upatikanaji wa taarifa zako iwe ni kwa njia ya kielectroniki au kwa njia ya mtu kwa mtu kuhakikisha unakuwa wa salama na wenye kufuata taratibu.
Ili tuweze hakikisha taarifa zako zinakuwa salama, ni muhimu pia kwako kuchukua tahadhali unapo sambaza kwa mtu mwingine taarifa zozote juu ya akaunti yako, kama vile neno la siri usimpe mtu mwingine na hakikisha unatumia neno la siri ambalo si rahisi mtu mwingine kuweza kulitambua, kama vile usitumie mwaka wa kuzaliwa kwenye neno la siri, usitumie jina lako au jina la ndugu yako n.k
Uwekaji wa taarifa zako salama ni moja ya wajibu wako muhimu kama mtumiaji, hatutowajibika kwa uvujaji, ubadhirifu au changamoto yoyote ile itakayosababishwa na mtumiaji kushindwa kuweka taarifa zake binafsi salama.
Vipi kuhusu Matanganzo?
Taarifa unazotupatia
Hizi ni taarifa unazo tupatia wakati wa usajiri, taarifa hizi ni kama majina yako, mawasiliano, anuani za makazi au stoo yako n.k.
Taarifa hizi ni kwa ajili ya kukutambua wewe kama mtumiaji na kurahisisha shughuli zako za kibiashara ndani ya mtandao wetu, hatuwezi sambaza taarifa hizi kwa mtu yeyote wa tatu.
Taarifa zikusanywazo na mifumo ya Stooyangu.com ®
Hizi ni taarifa ambazo zinakusanywa na mifumo ya Stooyangu.com ® wakati unapotumia kufanya shughuli zako za kibiashara, taarifa hizi zinaturahisishia sisi katika kufanya machagaguzi ya bidhaa uzipendazo na kuhakikisha tunakuletea bidhaa unazo zipenda wakati wote.
Hii inakurahisishia katika shughuli zako za manunuzi ukiwa kama mteja na uuzaji wa bidhaa ukiwa kama muuzaji.
Taarifa zikusanywazo ni kama aina ya bidhaa uzipendazo, stoo uzipendazo, bei unayopendelea n.k
Taarifa zikusanywazo kutoka vyanzo vingine
Hizi ni taarifa zinazo kusanywa kutoka kwa wadau wengine tunaofanya nao kazi ili kuhakikisha tunakuletea huduma uipendayo. Wadau hao wanaweza kuwa makampuni ya mitandao ya simu pale ufanyapo malipo ya bidhaa, makampuni ya usafirishaji wa bidhaa pale unapotumiwa bidhaa baada ya kukamilisha malipo.
Taarifa hizi zinatolewa au kupokelewa kwa umakini na kwa faragha kubwa ili kuepusha changamoto zozote zinazoweza jitokeza endapo taarifa hizo zikapokelewa na mtu asiye muhusika.
Haki yako juu ya taarifa zako
Ukiwa kama mtumiaji wa Stooyangu.com ® una haki zifuatazo juu ya taarifa zako:
Haki ya kuzifikia taarifa zako:
Ukiwa kama mtumiaji una haki ya kuzifikia taarifa zako zote tulizo ziifadhi bila kizuizi chochote kupitia mifumo yetu.
Haki ya kurekebisha taarifa:
Ukiwa kama mtumiaji una haki ya kurekebisha taarifa zako pale inapokubidi ikiwa taaratibu zote za matumizi ya mifumo yetu zimefuatwa.
Haki ya kutokukubali juu ya usambazaji wa taarifa zako:
Taarifa zako zinasambazwa kwa lengo zuri hususani ni katika kuhakikisha huduma tunazozitoa ni bora na rahisi kwako, ikiwa haujapendezwa kwa namna yoyote ile juu ya usambazaji wa taarifa zako, kama mteja una haki ya kutokukubaliana na swala hili na unaweza kuwasiliana nasi na kututeleza kuhusu maamuzi hayo.
Unaweza wasiliana nasi kwa taarifa zaidi:
E-mail: taarifa@stooyangu.com